22 Oktoba 2025 - 14:16
Source: ABNA
Kuonekana kwa athari za mateso makali kwenye miili ya mashahidi wa Palestina; "Uchunguzi uanze mara moja"

Taasisi moja ya kimataifa imetaka uchunguzi wa haraka uanze kuhusu mateso makali ya wafungwa wa Palestina yaliyofanywa na utawala wa Kizayuni.

Kulingana na shirika la habari la Abna likinukuu Russia Al-Youm, Shirika la Kimataifa la Haki za Binadamu la Ulaya-Mediterania limetangaza kwamba uchunguzi wa haraka wa kimataifa unapaswa kufanywa kuhusu athari za mateso zilizobaki kwenye miili ya mashahidi wa Palestina.

Taasisi hiyo ya kimataifa imesisitiza kuwa miili ya mashahidi 120 wa Palestina imekabidhiwa na utawala wa Kizayuni na athari za mateso makali na mauaji ya kiholela zinaonekana kwenye miili hiyo.

Taasisi hiyo imeeleza kuwa athari za kamba kwenye shingo za miili hiyo na risasi zilizopigwa kwao kutoka umbali mfupi ni wazi kabisa. Pia mikono na miguu yao ilikuwa imefungwa kwa waya, na baadhi ya miili hiyo ilitupwa chini ya vifaru. Mifupa yao imevunjika na kuna majeraha makali ya kuungua. Watu hawa hawakufa kifo cha kawaida, bali waliuawa kishahidi. Ni miili sita tu kati ya miili 120 iliyokabidhiwa iliyotambuliwa.

Your Comment

You are replying to: .
captcha